Leben fuer Tansania e.V.
& BrightStar Foundation

Bright Star Foundation - Swahili

Bright Start Foundation ni shirika lisilo la kiserikali lililopo Arusha, Tanzania. Shirika hili limeanzishwa na kusajiliwa tarehe 12 January mwaka 2013, kwa  nambari za usajili No. 00NGO/00006043. Bright Star Foundation ina lengo la kujenga ushirikiano na mashirika mengine pamoja na serikali katika kukabiliana na umaskini kwa kukuza maendeleo ya kijamii, haki za kiuchumi pamoja na uwepo amani.

Bright Star Foundation inahusisha mkakati wa taifa wa maendeleo na kupunguza umaskini hasa nguzo I na II zilizojikita katika kuboresha na kuimarisha hali ya maisha ya Watanzania. Shirika la BSF limekuwa na ushirika na taasisi zingine katika jamii kwa kufuata misingi husika iliokuwepo katika malengo ya maendeleo ya millennia na pia malengo mapya ya maendeleo endelevu.

 

TASWIRA.

Jamii endelevu zenye kumiliki ustawi wake.

 

DHAMIRA

Kuishawishi jamii kuwa na ari ya kujitoa, kujituma na kutambua uwezo wa kutumia rasilimali zinazopatikana kuleta maendeleo endelevu na maisha bora.

TUNAYOFANYA.

Ø Usaidizi katika elimu hasa kwa kutoa ruzuku ya mahitaji mbalimbali ya shule kwa wanafunzi wenye uwezo mkubwa wa kidato cha I-IV katika Wilaya za Arumeru na Arusha, lengo likiwa kukuza elimu kwa kuhimiza ustadi na uhitimu wa kidato cha nne.

Ø Kuwajengea uwezo na kuwawezesha wajasiriamali husika wenye jitihada na mipango madhubuti. Kukuza matumizi yenye tija na kuongeza thamani kwa rasilimali zinazopatikana ili kutengeneza mapato na kuboresha hali ya maisha.

Ø Utetezi dhidi ya ukatili (ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto). Kuhusisha maswala ya kisheria, utatuzi wa migogoro na ujenzi wa amani katika jamii husika pamoja na ushawishi katika maswala ya ustawi wa jamii na jitihada za kimaendeleo.

Ø Usaidizi kwa mtoto wa kike na uwezeshaji wa wanawake. Kuweka msisitizo katika elimu, maadili na utoaji bidhaa kama misaada kwa wahitaji.

Ø Kukuza ushawishi wa wanawake katika ukuaji na maendeleo ya jamii.

 

 

 

MATARAJIO

 

1.     Wanafunzi wenye uwezo mkubwa wanapata elimu na usaidizi kukidhi mahitaji mengineyo ya shule.

2.     Wajasiriamali wenye uelewa, utayari na uwezo wa kufanya biashara kiitaalam kupitia ushauri na mafunzo ya usimamizi wa biashara.

3.     Wajasiriamali wenye uwezo wa kukopesheka na kupata vifaa vyenye kukidhi uendeshaji wa biashara husika, kupitia mafunzo ya biashara, matumizi ya vifaa, fursa za huduma za kifedha pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi.

4.     Jamii zenye uwezo wa kusimamia sheria katika kuwasaidia walionusurika katika ukatili kwa kuripoti matukio na kushawishi ustawi wa jamii na ujenzi wa amani.

5.     Jamii zenye uwezo wa kutoa elimu ya jinsia na semina kuhusu afya na kujenga mifumo yenye kuhakikisha jamii inawajibika katika utatuzi wa ushawishi hasi wenye kuathiri ustadi wa wanafunzi kujifunza na maendeleo kwa ujumla.

6.     Wanawake wenye uwezo kupitia warsha mbalimbali zenye kuhimiza ujasiriamali unao ongozwa na wanawake au vikundi vyao.